Mshtarii

Image source
Mshtarii ni sayari ya tano kutoka Jua katika Mfumo wa Jua, na sayari kubwa kabisa ya mfumo. Tungamo yake inazidi mara mbili na nusu masi ya sayari nyingine zote pamoja. Wikipedia
Mshtuko wa moyo
Shtuko la moyo
Wikipedia
Mshubiri

Image source
Kwa kipimo chenye jina la karibu angalia hapa shubiri Mshubiri au msubili ni jina la mimea ya jenasi Aloe katika nusufamilia Asphodeloideae ya familia Xanthorrhoeaceae ambayo ni aina za sukulenti. Watu wengi wanaendelea kuweka Aloe ndani ya familia yake Aloaceae. Spishi kadhaa ni miti, lakini siku hizi huainishwa katika jenasi Aloidendron. Majani ya mishubiri na dawa zilizotengenezwa kutoka haya huitwa shubiri. Mimea hii ina shina fupi au haina shina kabisa, isipokuwa spishi zilizo miti. Majani ni marefu na manono na yanatoka shina karibu na wenziwe; yana miiba kingoni mwao. Maua yana umbo wa mrija mfupi na rangi yake ni nyekundu, pinki, ya machungwa, njano au nyeupe. Yapo mwishoni mwa kikonyo chenye vitawi au bila vitawi. Utomvu utokao mwenye majani hutumika kutengeneza dawa. Spishi moja inajulikana sana: mshubirimani (Aloe vera), ambao unapandwa sana duniani na hutumika kwa kutengeneza dawa za uganga au za mitishamba. Spishi nyingine inayopandwa sana katika Afrika na nchi nyingine za Tropiki ni mshubiri mwekundu (A. ferox). Wikipedia
Mshumaa

Image source
Mshumaa (kwa Kiingereza candle, kutokana na Kilatini candēla, neno ambalo linategemea kitenzi candēre, kuangaza.) ni kifaa cha kuletea mwanga gizani kinachotengenezwa kwa nta au kemikali fulani. Unaweza kuwashwa pia kwa sababu ya kuleta harufu au joto, au hata kwa kupima muda. Ili kushika mshumaa, tangu zamani vilitengenezwa vinara vya thamani tofautitofauti na hata vilivyopambwa kwa sanaa. Mshumaa unawashwa kwa kiberiti, halafu unaendelea wenyewe huku ukiyeyuka taratibu. Wikipedia
Mshumaa wa Pasaka

Image source
Mshumaa wa Pasaka au Mshumaa mkuu ni mshumaa maalumu unaotumika katika liturujia ya madhehebu mbalimbali ya Ukristo wa magharibi kama kiwakilishi cha Yesu mfufuka. Mshumaa mpya wa namna hiyo unabarikiwa na kuwashwa kila mwaka katika kesha la usiku wa Pasaka, halafu unawashwa wakati wa maadhimisho mbalimbali, kama vile yale muhimu zaidi ya Kipindi cha Pasaka (hadi Pentekoste) na hata nje yake, kwa mfano wakati wa ubatizo na mazishi ya Kikristo. Unatakiwa kuwa mkubwa kuliko mishumaa ya kawaida na uweze kudumu hadi Pasaka ya mwaka unaofuata. Kwa kawaida unachorwa alama mbalimbali, hasa msalaba wa Yesu na herufi za Kigiriki Alfa na Omega, ambazo ni ya kwanza na ya mwisho katika alfabeti ya lugha hiyo ya Agano Jipya, na hivyo zinamaanisha kuwa Kristo ni mwanzo (asili) na mwisho (lengo) wa ulimwengu wote. Baada ya kuwashwa kwenye moto wa Pasaka, mshumaa huo unapelekwa kwa maandamano hadi mimbarini, na wakati huo waamini wanawasha kwake mishumaa yao binafsi ili kumaanisha kwamba wameshirikishwa mwanga wa Kristo na kumfuata. Wikipedia
Mshume
Mshume Kiyate
Wikipedia
Mshume Kiate
Mshume Kiyate
Wikipedia
Mshume Kiyate

Image source
Mshume Kiyate alikuwa mwanaharakati na mzalendo aliyeshiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika katika miaka ya 1950. Vilevile alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa karibu sana na Hayati Mwalimu Nyerere hata kupelekea kumzungumzia mara kwa mara katika mazungumzo yake. Mwalimu siku moja katika kuwakumbuka rafiki zake wa zamani akizungumza na Dossa Aziz na wageni wengine nyumbani kwake Msasani, katika kuelezea kile alichokiita "the TANU spirit" yaani moyo wa upendo wa wana-TANU, alisema kuwa, siku moja wakati wa kudai uhuru alikuwa anatoka nyumbani kwake Magomeni akija Kariakoo kwa miguu kuelekea sokoni kutafuta mahitaji yake, lakini mfukoni alikuwa hana senti moja. Njiani akakutana na Mzee Mshume Kiyate. Alipomuuliza anakwenda wapi, alimfahamisha kuwa anakwenda sokoni lakini hana fedha za kununua chochote. Mzee Mshume aliingiza mkono katika koti lake na akatoa shilingi mia mbili akampa. (Ukitaka kujua thamani ya fedha hizo ikutoshe tu kuwa nyumba ya vyumba sita kujenga Kariakoo ilikuwa inagharimu shilingi mia tano). Kutokana na hali hii Mshume Kiyate aliona itakuwa ni kumtwisha Mwalimu mzigo mzito ikiwa atakuwa anashughulika na kuwatafutia wanawe chakula na wakati huo huo anafanya kazi za TANU. Mzee Mshume akajitolea kuihudumia nyumba ya Mwalimu kwa chakula. Alifanya hivyo hadi uhuru ulipopatikana. Baada ya uhuru Mwalimu alimwomba Mzee Mshume aache kufanya hivyo lakini alikataa na akamtafadhalisha Mwalimu aendelee kula chakula chake na kile ambacho kinatolewa na serikali kwake yeye kama mkuu wa nchi alimuomba Mwalimu awape wageni wake. Baada ya maasi ya wanajeshi wa KAR tarehe 20 Januari, 1964 kuzimwa na jeshi la Kiingereza, TANU ilifanya mkutano mkubwa sana Jangwani. Mzee Mshume kwa niaba ya wazee wa TANU alipanda jukwaani na kumvisha Mwalimu kilemba kama ishara ya kuunga mkono uongozi wake. Wikipedia
Msia
Msia ni kata ya Wilaya ya Mbozi katika Mkoa wa Songwe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 53304. Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 20,289 . Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 27,361 walioishi humo. Wikipedia
Msiba
Msiba (kutoka neno la Kiarabu: مصيبة) ni hali au tukio lolote la kusikitisha au la kuleta majonzi linalompata mtu binafsi au jamii, kama vile kifo cha ndugu, ajali, kufilisika n.k. Dini mbalimbali zinasaidia kukabili misiba inayoweza ikatokea maishani. Mara nyingi utamaduni kuhusu misiba unategemea dini ya wahusika. Wikipedia
Msichana

Image source
Msichana ni mwanamke ambaye hajafikia ukomavu wa utu uzima, ni kijana wa jinsia ya kike, ijapokuwa si tena mtoto tu wa binadamu. Wakati mwingine watu wakubwa bado hutaja kama 'wasichana' wanawake waliokua, hasa katika hali ya kutoka nao usiku katika starehe fulani. Wasichana wadogo bado wana miili ya kitoto. Haikomai hadi watakapofikia umri wa balehe (huenda wakafikia umri wa miaka 11-13 n.k.) ambapo miili yao inaanza kukomaa na kuwafanya wanawake kamili. Wakati wa kubalehe, msichana anaanza kuwa na maziwa, maumbo yake sehemu za kiunoni na mabegani yanakuwa kubwa, sauti na sura huwa nzuri inayovutia na anaanza kuwa na hedhi. Wikipedia
Msichana-Ajabu
Jean Grey
Wikipedia
Msigani
Msigani ni kata ya Wilaya ya Ubungo katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania, yenye postikodi namba 16114. Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 82,988 . Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 55,111 waishio humo. Wikipedia
Msikisi
Msikisi ni kata ya Wilaya ya Masasi katika Mkoa wa Mtwara, Tanzania, yenye postikodi namba 63546. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2022, kata ilikuwa na wakazi wapatao 8,172 . Wikipedia
Msikiti

Image source
Msikiti ni mahali pa ibada kwa waumini wa dini ya Uislamu, ambapo lengo kuu ni kutekeleza wajibu wa sala chini ya imamu. Hata hivyo ukumbi unaweza kutumika pia kwa kuelimishana na kujadiliana, kama ilivyokuwa kwa masinagogi ya Wayahudi. Waislamu wengi mara nyingi huita msikiti kwa kutumia jina la Kiarabu, ambalo ni masjid - مسجد — inatamkwa [ˈmæsʤɪd] (wingi wake ni: masajid kwa Kiarabu: مساجد — inatamkwa /mæˈsæːʤɪd/). Kutoka Uarabuni misikiti imeenea duniani kote, ikiunganishwa mara nyingine na minara. Baadhi yake inatumia sanaa ya hali ya juu. Wikipedia
Msikiti Mkuu wa Djenné
Msikiti Mkuu wa Djenné ni jengo kubwa la matofali au adobe katika mtindo wa usanifu wa Sudano-Sahelian. Msikiti huu uko katika mji wa Djenné, Mali, kwenye uwanda wa mafuriko wa Mto Bani. Msikiti wa kwanza kwenye eneo hilo ulijengwa karibu na karne ya 13, lakini muundo wa sasa ulijengwa mwaka 1907. Mbali na kuwa kitovu cha jamii ya Djenné, ni moja ya alama maarufu zaidi barani Afrika. Pamoja na "Miji ya Kale ya Djenné", uliteuliwa na UNESCO kuwa kituo cha Urithi wa Dunia mwaka 1988. Wikipedia
Msikiti Mkuu wa Kilwa
Msikiti Mkuu wa Kilwa Ni msikiti wa sharika katika kisiwa cha Kilwa Kisiwani, katika Mji wa Kilwa Masoko Wilaya ya Kilwa katika Mkoa wa Lindi nchini Tanzania. Inawezekana ilianzishwa katika karne ya kumi, lakini hatua kuu mbili za ujenzi ni za karne ya kumi na moja au kumi na mbili na kumi na kwa mtiririko huu.Ni miongoni mwa misikiti ya mwanzo iliyosalia katika pwani ya Uswahilini na ni miongoni mwa misikiti ya kwanza kujengwa bila ua. Ni ukumbi mdogo wa maombi wa kaskazini ulianza awamu ya kwanza ya ujenzi na ulijengwa katika karne ya 11 au 12.Ilikuwa na jumla ya ghuba 16, zikiungwa mkono na nguzo tisa, ambazo awali zilichongwa kutoka kwa matumbawe lakini baadaye zikabadilishwa na mbao.Muundo huu, ambao ulikuwa umeezekwa paa, lulikuwa mmoja wa misikiti ya kwanza kujengwa bila ua. Ilirekebishwa katika karne ya 13 na kuongeza nguzo za kando, mbao, mihimili inayopita. Wikipedia
Msikiti wa Gaddafi
Msikiti wa Gaddafi, Dodoma
Wikipedia
Msikiti wa Gaddafi, Dodoma

Image source
Msikiti wa Gaddafi ndio msikiti mkubwa zaidi nchini Tanzania na wa pili kwa ukubwa Afrika Mashariki baada ya Msikiti wa Kitaifa wa Uganda nchini Uganda. Uko katika mji mkuu wa Tanzania wa Dodoma. Uko katika majira nukta 6.172689°S 35.745721°E / -6.172689; 35.745721 Ulipewa jina la Kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi ambaye alitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wake kupitia Jumuiya ya Ulimwengu ya Miito ya Kiislamu. Msikiti huo ulizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2010 na una uwezo wa kuchukua waumini wasiopungua 3,000. Wikipedia
Msikiti wa Ijumaa, Mji Mkongwe
Msikiti wa Ijumaa ni msikiti uliopo Mji Mkongwe, Zanzibar, Tanzania. Msikiti huo ulikarabatiwa kabisa mwaka wa 1994 kwa mtindo wa kisasa wa arabesque. Wikipedia