You are on page 1of 10

KITINI CHA

MAFUNZO

YA

UJASILIA MALI KWA

VITENDO

NA MAMA IRENE
YALIYOMO

UTANGULIZI:

SHUKRANI:-

SURA YA KWANZA
• UTENGENEZAJI SABUNI ZA MAJI
• SABUNI ZA KUNAWIA MIKON O
• SABUNI ZA CHOONI
• SABUNI ZA KUFULIA
• SHAMPOO
• UTENGENEZAJI SABUNI ZA MICHE

MAFUTA YA MGANDO (Kupaka )

SEHEMU YA PILI

UTENGENEZAJI WA :

• BATIKI AINA ZOTE


• UTENGENEZAJI VIKOI
• SHANGA, HERENI, BANGILI
• UTENGENEZAJI ZURIA

SEHEMU YA TATU

UTENGENEZAJI VITAFUNWA

• MAANDAZI
• SKONZI
• KARANGA ZA MAYAI
• TAMBI

UTENGENEZAJI SABUNI ZA MAJI

AINA ZA SABUNI.

i. Sabuni za kunawia mikono


ii. Sabuni za usafi wa chooni
iii. Sabuni za kufulia.
JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI ZA KUNAWIA MIKONO MALIGHAFI

1. Sulphonic asid - Inafanana na asali


2. Siless - Kuimarisha povu la sabuni,sabuni iwe imara
3. Sodaash - Inang'arisha sabuni,kuongeza povu
4. Formalinge - kuuwa bacteria, sabuni kukaa kwa muda mrefu.
5. Rangi - Kuongeza uzito wa sabuni
6. Maji -Kibebeo inabeba sabuni yote
7. Griseline - Inarainisha ngozi, mikono
8. Perfume -Inaleta harufu nzuri ya sabuni/
9. Chumvi

HATUA ZA KUTENGENEZA

1. Maji lita 10 yaliyochujwa


2. Sulphonic acid vijiko 3 vya chakule
3. Koroga kwa dakika 5-15 kulia au kushoto
4. Siless ½ lita weka kwenye mkoroho changanya koroga
5. Formalinge kyiko 1 cha chakula koroga
6. Griseline vijiko 3 vya chakula koroga
7. Rangi ½ kijiko cha chai koroga /kijani/Bluu
8. Sodaash vijiko 2 vya chai weka katika sabuni koroga
9. Chumvi Robo 3 koroga pembeni mimina, endelea kukoroga chumvi inaleta uzito kwenye sabuni
endapo itakuwa nzito zaidi ongeza maji koroga.
10. Perfume weka vijiko 2 vya chakula koroga tayari kwa matumizi iache ipoe kwa masaa 2 na
fungasha kwenye vifungashio.

NB. Funika sabuni kuzuia harufu perfume kupotea.

SABUNI YA CHOONI

MALIGHAFI

1. Maji lita 10.


2. Sulphonic asid ½
3. Siless vijiko 5 vya chakula
4. Formalinge vijiko 5
5. Chumvi ¼ ilo, kuongeza uzito
6. Sodaash vijiko 4 vya chakula
7. Rangi kijiko 1 cha chakula
8. Perfume vijiko 2 vya chakula

JINSI YA KUTENGENEZA/ HATUA ZA KUTENGENEZA

1. Weka maji lita 10.


2. Sulphonic acid 1/2 lita.
3. Siless - vijiko 5 vya chakula
4. Formaline vijiko 5 vya chakula
5. Rangi kijiko 1 cha chakula
6. Chumvi 1/4 kilo
7. Sodaash vijiko 4 vya chakula
8. Perfume vijiko 2 vya chakula
Koroga dakika 20-30 na uhakikishe hakuna weupe wa mabonge ndani ya dawa yako.

NB: Funika acha kwa masaa 2 ipoe weka kwenye vifungashio.

SHAMPOO

MALIGHAFI

i. SULPHONIC ASID - Inaongeza pavu


ii. SODAASH - Kukata asid
iii. MAJI
iv. SLESS - Huongeza povu na kung'arisha
v. FOMALINE - Kwa ajili ya kuuwa wadudu
vi. GRYCELINE -Kuleta umafuta
vii. PERFUME/HARUFU NZURI YA KUNUKIA
viii. CHUMVI YA MAWE - Kuleta uzito.

JINSI YA KUTENGENEZA . SHAMPOO


Andaa ndoo au beseni na malighafi fuata mtiririko ufuatao:

• Maji lita 10
• Sulphonic asid vijiko 4 vya chakula
• Silesi ½ kg koroga kwa dakika 15
• Sodaash vijiko 2 vya chakula endelea kukoroga
• Griseline vijiko 5 vya chakula koroga
• Fomaline vijiko 4 vya chai
• Rangi ¼ kijiko cha chai (kijani,bluu)
• Chumvi ¼ koroga
• Kiini cha mayai 2 koroga pembeni na maji ya sabuni dk 15 changanya koroga
• Perfume vijiko 3 vya chakula
• Shampoo iwe nzito
• Funika Shampoo iache muda wa masaa 2 tayari kwa matumizi paki kwenye vifungashio tayari
kwa kuuza.

UTENGENEZAJI SABUNI ZA MCHE

(sabuni za magadi au Gwanji)

1. Kuna sabuni ambazo zinaharufu (perfumu) na ambazo hazina


Povu jingi la kutosha
Iwe haina mwasho
Rangi (bluu)
Iwe ngumu
Iwe imara
Iwe na shepu nzuri inayoweza kuvutia mteja.

MALIGHAFI
1. Cost soda(itunzwe juu ya kitu kama mbao ukiweka chini inaganda
11. Mafuta, Mbosa,(Mise), mawese,kolie,alizeti.
Hydrogen peloc side - kugeuza mafuta, sabuni kuwa nyeupe ing'ae kuipa imara
Sodiam silicate- kuondoa muwasho.
Hydrometer- kifaa kinachotumika kupima kiwango cha joto kinatakiwa kiwe kuanzia nyuzi joto 28 hadi
30
Meza hutumika kukatia sabuni
Box, umbo la sabuni , box la mbao hutengenezwa kwa kufuata vipimo vya sabuni ni urefu, upana na kina
.
Kisu ,kamba, karatasi la nailoni kuzuia uji wa sabuni usivuje endapo box lina matundu.

JINSI YA UTENGENEZAJI SABUNI ZA GWANJI/MCHE


MALIGHAFI

Mafuta lita 20
Maji yaliyochanganywa na costic soda lita 10
Bluu vijiko 6 vya chakula
Vaa glovus
Maxic/puani
Gamu boot.

JINSI YA KUCHANGANYA COSTIC NA MAJI


Pima maji lita 10
Cost soda lita 4kg
Koroga maji na costic mpaka iyeyuke costic, koroga kwa muda wa dakika 40-45 kwa kutumia
mwiko mrefu.

ANGALIZO

Hakikisha umevaa vifaa tajwa hapo juu.


Hakikisha unakorogea mahali palipo na hewa ya kutosha costic ni hatari sana, hakikisha isikirukie wakati
wa kukoroga pia hakikisha usishike kwa mikono mitupu kama imetokea imekudondokea bahati mbaya
osha kwa maji haraka sana.

HUDUMA YA KWANZA

Maji
Baada ya kukoroga kwa dakika 40 - 45 utaiacha kwa muda wa masaa 24

ANGALIZO
Weka sehemu isiyoingiwa na watu mara kwa mara ni hatari.
Baada ya kupoa unachukua kipimo ambacho ni Hydrometer temprecher ni kipimo kinchopima
joto hakikisha Hydrometer imesoma nyuzi joto 280,29 -30.

JINSI YA KUFANYA

Andaa box la mbao


Karatasi ya mpira ya bluu - mita 2 1/2 Ndoo kubwa 2 na dyaba .
Chukuwa mafuta lita 20 unamimina kwenye ndoo kubwa, mafuta yaliyoyeyuka sio mgando.
Chukua maji yaliyochanganywa na costic soda yenye nyuzi joto 30? unamimina kwenye ndoo
yenye mafuta , unamimina kidogo kidogo huku mtu mwingine akiendelea kukoroga kwa kutumia
mwiko mrefu, koroga kwa dakika 30 huku ukiwa unaandaa box umeliwekea karatasi ndani ya
prastic /mpira. Baada ya dakika 30 kuisha utamimina uji uliokoroga kwenye box hilo. Baada ya
kumimina utaweka rangi.

JINSI YA KUWEKA RANGI.


Rangi ya bluu
Rangi ya mafuta
Chukua mafuta kidogo robo lita
Pima vijiko 6 vya chakula vya rangi ya bluu
Changanya na mafuta robo lita koroga mpaka ilainike pembeni.
Changanya, mimina kwenye box lenye uji huku ukiwa na kibao kirefu kama fimbo una kata
mistari ili kuweka mawingu.
Acha ipoe kwa muda wa masaa 24 . Baada ya masaa 24 sabuni iko tayari kwa matumizi!.
Kijiko cha chakula
Beseni la plastic, ndoo
Gloves, mask, mkasi,meza, mkaa, kuni

AINA ZA BATIKI

Kufinyanga
Kufunga
Kukunja
Box au Tofali

JINSI YA KUTENGENEZA

Andaa kitambaa mita 3 kwa dizaini unayotaka


Andaa maji ya moto
Changanya sodium. Caustic, rangi na black fixcer gm 30 kwa mita 3 au 4 Weka kitambaa chako
kwenye mchanganyiko huo huku ukigeuza geuza kwa muda wa dakika 15
Ondoa kitambaa chako kwenye mchanganyiko huo weka juu ya kamba
Toa juu ya kamba weka kwenye beseni lenye maji baridi fua na suuza baada ya hapo anika juani.
Kikikauka piga pasi tayari kwa kuuza.
BATIKI ZA BLEACH
MALIGHAFI

Kitambaa cha plain wax 6 mita


Blichi ya maji
Maji ya kawaida

JINSI YA KUTENGEZA

Chukua maji 1/2 kikombe


Changanya nab rich vifuniko 3
Hakikisha unachanganya vizuri na maji yanateleza baada ya kuweka brich.
Funga kitambaa au nyunyiza sehemu ulizo funga au ulizolenga
Acha dk 10 kisha fungua mafundo kama ulifunga na kama ulinyunyiza weka kwenye maji safi.
Suuza kwenye maji ya baridi kasha anika kivulini.
Piga pasi tayari kwa kuuza

NB: Batiki zipo za aina nyingi waweza kutengeneza Batiki za printi kwa kutumia mishumaa na
kugonga maua mbalimbali kwa kutumia vibao.

UTENGENEZAJI VIKOI
MALIGHAFI

Vikoi
Shanga (rangi, bluu,nyeupe, nyekundu, njano n.k.)
Uzi
Mkasi
Sindano (spesho kwa ajili ya kutungia shaga)
Vitambaa kwa ajili ya kuchorea picha za wanyama mbalimbali Kiberiti cha gesi.

JINSI YA KUTENGENEZA

Andaa kikoi kwa saini unayotaka Fumua pande mbili ili kusokota kikoi (urembo)
Sokota kwa kufuata saizi moja ili kuleta mlinganyo sahihi wa urembo wako. Tunga uzi kwenye
sindano
Ingiza shanga kwa rangi ulizokusudia na anza kushona kwa kuchoma juu juu ili kuzuia uzi
kuonekana kwa ndani.
Unapomaliza choma sehemu za nyuzi zilizojitokeza kwa kutumia kiberiti cha gesi pia waweza
kubandika picha za wanyama kwa kudalizi ukipenda.

MAMBO YA KUZINGATI

Panga shanga kwa mahesabu (kuhesabu ili kuleta mchanganyiko mzuri wa rangi
ulizokusudia .
Sindano za shanga ni nyembamba sana, tunza vizuri tumia kwa uangalifu kuepuka
kuvunjika kwa sindano
Unapochora michoro ya maua, tumia chaki ili kukusaidia kuona vizuri wakati wa kushonelea
shanga pia unapobandika picha za wanyama weka alama kwa kutumia chaki nyeupe.

UTENGENEZAJI WA SHANGA, HEREN BANGILI

MALIGHAFI

Sindano
Uzi Shanga (mbalimbali)
Waya uliojikunja kwa ajili ya kutungia shanga
Nozo Mkasi

UTENGENEZAJI WA ZURIA

MALIGHAFI
Sindano (spesho)
Mfuko wa gunia safi
Mkasi
Uzi
Maorkapen (kwa ajili ya kuchorea maua).

NB: Elimu ya vikoi, shanga, bangili, herein ni kwa vitendo hivyo wasiliana nami kwa namba hii
0768 534 698 ujifunze kwa vitendo uweze kuelewa vizuri.

SEHEMU YA TATU
UTENGENEZAJI WA VITAFUNWA

MAANDAZI

Ngano 1kg
Sukari ¼ kg
Baking powder kijiko kimoja cha chakula
Amira kijiko 1 cha chakula
Rangi ya chakula kijiko 1 cha chai Mafuta kiasi kwa ajili ya kukandia
Chumvi kidogo (ukipenda)
Vanila ukipenda yanakuwa na radhi nzuri.

HATUA

Umua Amira pembeni kwenye kikombe iumuke


Changanya vitu vyote anza kukanda kanda mpaka unga wote uchanganyikevizuri na usiwe
mgumu sana.
Baada ya kukanda vizuri, funika kwa karatasi ya nailoni au chombo kikavu uumuke kwa muda wa
dakika 20.
Weka kwenye meza anza kusukuma bonge la unga liwe mfano wa umbo la chapatti katakata
kwa saizi unayotaka.
Andaa kikaango moto wa wastani ili mandazi yaive bila kuungua.

UTENGENEZAJI WA SKONZI
MALIGHAFI

Ngano kilo 1 kg
Amila kijiko 1 cha chakula
Mayai 2
Maziwa 1/4 kikombe (ukipenda) Sukari vijiko 4 vya chai Chumvi kidogo.

HATUA

Umua Amila
Gonga mayai kwenye bakuli pembeni pigapiga kwa kijiko yachanganyikane vizuri.
Changanya vitu vyote na anza kukanda mpaka unga uchanganyike vizuri. Weka maziwa ya
uvuguuvugu yaliyochanganywa na maji, weka maziwa kidogo kidogo huku ukiendelea kukanda
unga. Kata mabonge mabonge kama ya chapati.
Andaa sufuria, paka mafuta ndani.
Weka mabonge,funika na mfuniko wa bati acha yaumuke
Baada ya kuumuka weka kwenye jiko moto chini wa wastani juu weka mwingi kiaisi. Kuhakikisha
kama zimeiva choma kijiti ukiona unga haung'anganii basi zitakuwa tayari
Acha zipoe kwa muda, weka kwenye vifungashio au tumia kwa kula.

UTENGENEZAJI KARANGA ZA MAYAI


MALIGHAFI

Mayai - 2
Sukari - 1/4 kg Ngano -1/4 kg Karanga - 1 kg
Mafuta ya kula (kupikia)

HATUA

Andaa bakuli gonga mayai changanya na sukari koroga weka chumvi kiasi koroga hakikisha
sukari na chumvi vimeyeyuka.

Weka karanga ulizochambua vizuri ndani ya bakuli lenye Mkorogo huo kisha nyunyiza unga wa
ngano kidogokidogo hakikisha kila punje ya karanga imepata rojo na unga wa ngano.

Andaa sufuria au karai weka mafuta yachemke moto wa wastani tumbukiza karanga zichemke
katika mafuta hakikisha zinaiva na kuwa rangi kahawia zisiungue ipua na wekakwenye chombo
chenye matundu (chujio) ili kuchuja mafuta. ? Acha zipoe, tayari kwa kuliwa au kuuza.

TAMBI MAHITAJI

Unga wa dengu 1kg


Baking powder kijiko 1 cha chakula
Pilipili mbuzi 1 kama utapenda
Chumvi
Pilau masala ya unga kijiko 1 cha chai
Mashine ya kutolea tambi.
Jiko, mafuta , sufuria , karai .

HATUA

Kanda mchanganyiko wako kupata uji mzito kwa kutumia mikono hakikisha wote
umechanganyikana vizuri

Andaa jiko mafuta yaive kwa wastani

Weka unga kwenye mashine ya tambi anza kuzungusha mashine

Hakikisha unaweka tambi kiasi ili ziweze kuiva vizuri na tumia karai au sufuria iwe pana .

Tambi zikiiva weka kwenye chujio mafuta fungasha peleka sokoni.

HITIMISHO

Asante kwa kununua kitini hiki wewe unayesoma zingatia hatua zote katika ujifunzaji . Mungu
akuzidishie Baraka tele zenye mafanikio THUBUTU UTAONA MAFANIKIO

NB: Natoa Elimu ya ujasiliamali kwa mtu mmoja moja na kwa vikundi.

Wasiliana name kwa namba: +255 758 558 071

MAMA IRENE

You might also like