Matendo Quotes

Quotes tagged as "matendo" Showing 1-3 of 3
Enock Maregesi
“Watu hubariki wenzao ambao ni wakarimu, na hulaani wenzao ambao ni wabahili. Ukiwa mkarimu kwa watu umekopa neema kutoka kwa Mungu, na Mungu atakulipa kutokana na matendo yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kila mtu ana tabia, matendo, mawazo na akili yake tofauti na mtu mwingine hapa duniani. Usimdharau mtu ukidhani ana akili kama za kwako au anafikiri kama unavyofikiri wewe kwani kila mtu aliumbwa kivyake na Mwenyezi Mungu. Unaweza kudhani unamjua mtu kumbe humjui. Heshimu kila mtu kama unavyojiheshimu kwa sababu, kila mtu ni wa pekee. Kama tunavyotofautiana katika vidole na macho ndivyo tunavyotofautiana katika tabia, matendo, mawazo, imani, maadili na akili. Usimdharau mtu usiyemjua au unayedhani unamjua.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Uzima wa milele si mchezo wa kubahatisha! Kila mtu atalipwa kulingana na matendo yake, mema au mabaya, na huo uzima wa milele atapewa yule atakayetenda mema maisha yake yote.”
Enock Maregesi