Serikali Quotes

Quotes tagged as "serikali" Showing 1-18 of 18
Enock Maregesi
“Badilisha tabia. Badilisha mazingira ya maisha yako. Haijalishi una umri kiasi gani au wewe ni mwanamke au mwanamume, bado hujachelewa kubadili maisha yako kutoka duni kuwa bora – kuwa na amani, furaha na kuridhika. Kama desturi yako ni kuamka saa 12:00 asubuhi kila siku ili ufike kazini saa 2:00 asubuhi ambao ni muda wa serikali wa kuanza kazi, amka saa 11:30 asubuhi ili ufike kazini saa 1:30 asubuhi – nusu saa kabla ya kuanza kazi. Kama unafanya kazi ya taaluma uliyosomea lakini maisha hayaendi, fikiria kubadili mwelekeo wa maisha ikiwemo taaluma kufikia malengo uliyojiwekea.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wananchi wakiamua kufanya kitu katika nchi yao kwa asilimia 100 serikali, na taasisi zake zote, haitaweza kuwazuia. Kwa sababu, mamlaka ya wananchi hushinda ya serikali.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wananchi wataendelea kuwepo hata kama serikali haitakuwepo. Serikali haiwezi kuwashinda wananchi. Sauti ya umma ni sauti ya Mungu. Serikali haiwezi kumshinda Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kitalifa ni utiifu kamili, woga, umbali (kwa maana ya kuwa mbali na biashara ya mamafia wengine mpaka kwa makubaliano maalumu) na nidhamu ya kutoshirikiana na mamlaka zote za serikali. Ukishtakiwa kwa kosa la madawa au ujambazi ambalo hukufanya, utatumikia kifungo mpaka mwisho bila kushirikiana na polisi (kwa maana ya kutaja aliyehusika au waliohusika na uhalifu huo) hata kama aliyehusika au waliohusika hana au hawana uhusiano wowote na Kolonia Santita. Falsafa ya Kitalifa ni Sheria ya Kitalifa ya Kiapo cha Swastika cha Kolonia Santita. Na adhabu ya kuvunja sheria hiyo ni kifo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Serikali mara nyingi hutegemea ujasusi wa ndani na nje kufanya maamuzi mazito na sahihi ya kuendesha nchi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukanda wa Gaza ni jimbo lenye miji minne na kambi mbalimbali za wakimbizi za Umoja wa Mataifa – lenye urefu wa kati ya kilometa 41 au maili 25 na lenye upana wa kati ya kilometa 6 mpaka 12 au maili 3.7 mpaka 7.5, pamoja na eneo la jumla la kilometa za mraba 365 au maili za mraba 141. Jimbo hili liliwahi kutawaliwa na Wamisri, Wakaanani, Waisraeli, Wasiria, Wababelonia, Wagiriki, Warumi, Waturuki, Waingereza, na Wapalestina, na limekuwa uwanja wa vita kwa karne nyingi kwa sababu za kidini na kihistoria. Ukanda wa Gaza uko chini ya Palestina. Uko chini ya serikali ya Hamas.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Yusufu alikuwa hohehahe kabla na baada ya kuuzwa na nduguze kama mtumwa nchini Misri. Hakuwa na pesa, hakuwa na elimu, hakujuana na viongozi wa serikali. Lakini kwa vile alikuwa na Mungu, Mungu alimbariki mpaka watu wote wakashangaa. Yusufu alikuwa maskini ili mimi na wewe tuwe na tumaini leo, kwamba tukiwa na Mungu katika maisha yetu hatutatafuta utajiri. Utajiri ndiyo utakaotutafuta sisi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Serikali haibabaishwi na huruma. Inababaishwa na akili.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Serikali haishirikiani na huruma katika kufanya maamuzi yake. Inashirikiana na akili.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Serikali haiendeshwi na huruma. Inaendeshwa na akili.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mwananchi akitoa taarifa nyeti kwa serikali asisalitiwe kwa namna yoyote ile na serikali hiyo, na serikali ikitoa taarifa nyeti kwa mwananchi isisalitiwe kwa namna yoyote ile na mwananchi huyo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Serikali hutambua watu wanaojitambua.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wakati unaokubalika ni sasa. Ukijitambulisha utatambulika, usipojitambulisha hutatambulika. Serikali haitambui wahuni.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Usipojisajili BASATA watasema una kiburi. Serikali hupenda watu iliyoridhika nao. Wasanii wote nendeni BASATA mkajisajili.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kupeperusha bendera ya taifa kwa niaba ya taifa bila kujisajili serikalini ni kosa la jinai, na serikali haitakutambua kwa sababu wewe mwenyewe hujajitambua.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mambo madogomadogo yanayohusu serikali si ya kudharau. Kama unavyoona umuhimu kukata leseni ya gari lako, ona umuhimu hivyohivyo kujisajili serikalini.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiichukia serikali yako umeichukia nafsi yako. Kwa sababu serikali ndiyo inayoongoza nchi, na nchi ni mwili mmoja.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuipinga serikali si kuichukia; bali ni ombi la kutaka ibadilike.”
Enock Maregesi