Matatizo Quotes

Quotes tagged as "matatizo" Showing 1-30 of 33
Enock Maregesi
“Nukuu ya mwandishi wa vitabu wa Brazili, Paulo Coelho, "Tunapopenda tunajitahidi siku zote kuwa wazuri zaidi kuliko jinsi sisi wenyewe tulivyo. Tunapojitahidi kuwa wazuri zaidi kuliko jinsi sisi wenyewe tulivyo, kila kitu katika maisha yetu kinakuwa kizuri hali kadhalika.", inadhihirisha kikamilifu tabia ambayo bibi yangu (Martha Maregesi) alijitahidi kuwa nayo katika kipindi cha maisha yake yote. Alikuwa mtu mwenye furaha sana. Alikuwa na tabasamu lenye kuambukiza ambalo marafiki na familia yake hawakuweza kujizuia kutabasamu pia alipofurahi nao. Pamoja na kwamba alikumbana na matatizo mengi na bahati mbaya nyingi katika maisha yake, alijulikana kama mtu mwenye upendo na uvumilivu mkubwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu ni mwingi wa hekima, lakini kwa nini alimuumba Shetani? Kwa sababu, Shetani wakati mwingine ni hekima. Ukiendelea kupigwa, bila wewe kupiga, unaweza kuumia, familia yako inaweza kuumia pia! Kuepusha matatizo ya familia yako, wakati mwingine unahitaji kupigana.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna ndoto za mchana na kuna ndoto za usiku. Ndoto za mchana ni maono ya kile ambacho roho inatamani kuwa. Ndoto za usiku ni maono yanayotokea wakati akili imetulia baada ya mwili wote kupumzika. Ukiota kuhusu moto, hiyo ni ishara ya hasira; ukiota kuhusu maji, hiyo ni ishara ya siri; ukiota kuhusu ardhi, hiyo ni ishara ya huzuni; ukiota kuhusu Yesu, hiyo ni ishara ya mafanikio. Kitu cha kwanza kufanya unapoota ndoto za kishetani, utakapoamka, mwombe Mungu akunusuru kutoka katika matatizo yoyote yanayokunyemelea; au yanayomnyemelea mtu mwingine yoyote yule, hata usiyemjua. Ubongo ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni na umetengenezwa na Mungu. Ndoto zinapatikana ndani ya ubongo. Ubongo unapatikana ndani ya ufahamu. Ufahamu mtawala wake ni malaika mwema. Malaika mwema anajua siri ya ndoto. Kila mtu anaota na kila ndoto ina maana yake. Rekodi ndoto zako kila siku kwa angalau mwezi mzima kupata maana halisi ya ndoto hizo, na kujua kwa nini ulizaliwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mwili wako una uwezo wa kujua kabla yako kitakachotokea baadaye. Kama una njaa kwa mfano, mwili wako utakwambia. Kama una kiu, mwili wako utakwambia. Kama unaumwa, mwili wako utakwambia. Kama kuna kitu kibaya kinatarajia kutokea katika maisha yako au katika maisha ya mtu mwingine, mwili wako utakwambia. Kuwa makini na alamu zinazotoka ndani ya mwili wako, kwani hizo ni ishara za Roho Mtakatifu kukuepusha na matatizo ya dunia hii.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hakuna shaka yoyote (kwa mfano) kwamba mboga za majani na matunda vina vitamini nyingi mwilini na madini na vitu vyote vizuri katika mwili wa binadamu, na kwamba kadhalika vina kirutubisho cha ufumwele ambacho huzuia kufunga choo na matatizo mengine ya mfumo wa usagaji chakula. Kirutubisho hiki kikizidi mwilini utapata matatizo makubwa yatakayoweza hata kukusababishia kifo!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiona kitu ambacho hukupaswa kuona, au ukisikia kitu ambacho hukupaswa kusikia, fumba macho kwa kuyakodoa! Ulichokiona au kukisikia usikiseme leo na hata milele. Jifanye hukuona kitu, hukusikia kitu. Ukifumbua macho kwa kuyakodoa utapata matatizo, makubwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maisha yangu ni darasa. Jifunzeni kutokana na maisha yangu, jifunzeni kutokana na sifa zangu za ushupavu, jifunzeni kutokana na sifa zangu za udhaifu, kutatua matatizo katika maisha yenu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama John Doe ana matatizo katika maisha yake acha ayatatue mwenyewe. Akishindwa atakuomba ushauri au ataomba ushauri kutoka kanisani kama ni Mkristo, au msikitini kama Mwislamu, au kutoka katika nyumba yoyote ya ibada kulingana na imani yake. Mtu akikuomba ushauri mshauri kwa moyo wako wote, wala usimshauri kwa unafiki au kinyongo cha aina yoyote ile.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mapenzi, kama ilivyo kwa vitu vyote hapa ulimwenguni, hayawezi kuwepo bila kujumuishwa na fizikia na kemia yake! Bila kemia hakuna mapenzi ya kudumu. Tamaa ya ngono kimsingi huanza pindi unapokutana na mtu. Tamaa hiyo huweza kukua na kuwa kitu kingine kadiri muda unavyokwenda lakini chanzo kinakuwepo toka siku ya kwanza mlipokutana. Kemikali inayosababisha tamaa ya ngono na hata kuikuza tamaa hiyo ni 'phenyl ethylamine' ('fino itholamine') au PEA ambayo ni kemikali ya mapenzi ndani ya ubongo. Husisimua watu na huongeza nguvu za kimwili (fizikia) na kihisia (kemia). Tamaa husababisha mtu azalishe PEA nyingi zaidi, kitu kinachosababisha kujisikia kizunguzungu (cha hisia za kimapenzi) na dalili zingine kama magoti kutetemeka, jasho kutoka viganjani na kutokutulia. Kemikali hii inapozalishwa kwa kiwango kikubwa, hutuma alamu ('signals') kutoka kwenye ubongo mpaka kwenye viungo vingine vya mwili na kutumika kama 'dopamine' au 'amphetamine' ambazo ni kemikali za ulevi ndani ya ubongo. Iwapo unajiuliza kwa nini wewe au mtu mwingine unavutiwa na mtu ambaye hamwendani kimapenzi, inaweza kuwa ni kwa sababu una kiwango kikubwa cha kemikali hizo kuliko mwenzako, kitu ambacho huzidi uwezo wa kutumia kichwa na kutoa maamuzi bora kulingana na akili ya kuzaliwa.

Kwa jumla, mapenzi yote ya kweli uhitaji angalau kiwango kidogo cha PEA kwa wale wanaopendana. Cha msingi kukumbuka ni kwamba kemikali hizi huja kwa vituo, nikiwa simaanishi kwamba tamaa ya ngono hupotea pale mtu anapoelekea kwenye uhusiano wa kudumu. Lakini mambo hubadilika. Hatuwezi kuvumilia zile hisia kali kadiri tunavyozidi kusafiri kuelekea kwenye uhusiano wa kudumu na kwenye maisha ya pamoja yenye furaha. Katika uhusiano wenye afya hata hivyo matatizo hutokea hapa na pale. Chanzo cha Murphy na Debbie kupendana kilikuwa kemia zaidi kuliko fizikia. Kama hakuna kemia hakuna mapenzi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Unapokuwa na matatizo makubwa katika maisha, Shetani anakuandama sana, Mungu ana mpango maalumu na maisha yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Unapokumbana na matatizo makubwa katika maisha yako ujue Mungu ana mpango maalumu na maisha yako. Ndiyo maana Shetani anakuandama hivyo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani hataacha kukuandama. Atakuandama mpaka siku utakapookoka. Yaani, siku utakapookolewa na Yesu Kristo, siku ambapo Shetani hatakuwepo tena. Silaha kuu tunayotakiwa kuwa nayo ni imani. Mungu hababaishwi na matatizo yako. Anababaishwa na imani yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maskini ni mdogo kuliko matatizo yake. Tajiri ni mkubwa kuliko matatizo yake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Dunia imekata tamaa. Matatizo ya watu yamekuwa makubwa kuliko ukombozi wa maisha yao. Sekunde moja ya toba inaweza kukupa ufalme wa mbinguni. Hujachelewa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Matatizo ya watu yamekuwa makubwa kuliko Injili. Mungu hasisimuliwi na matatizo yako. Anasisimuliwa na imani yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukifanya maamuzi kubaliana na matatizo yake yote. Fanya kile ulichosema utafanya, hata kama sehemu ya kile ulichosema utafanya uliinukuu kutoka kwa wengine, hata kama watu hawatakubaliana na wewe.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Dunia huzunguka kwenye mhimili wake na huzunguka jua. Jua huzunguka kwenye mhimili wake na huzunguka falaki. Dunia hutumia takriban siku moja kuzunguka kwenye mhimili wake, na hutumia takriban mwaka mmoja kuzunguka jua. Jua hutumia takriban siku ishirini na tano kuzunguka kwenye mhimili wake, na hutumia takriban miaka milioni mia mbili na hamsini kuzunguka falaki. Yoshua alisimamisha jua ili lisizunguke kwenye mhimili wake na lisizunguke falaki. Kwa sababu jua lilisimama, kila kitu kilichoathiriwa na jua hilo kilisimama pia ikiwemo dunia. Hata hivyo, kwa sababu tukio la Yoshua kusimamisha jua na mwezi yalikuwa maajabu kutoka kwa malaika wema, malaika wema ndiyo wanaojua kwa hakika nini kilitokea. Yoshua alikuwa sahihi kusema jua lisimame si dunia isimame. Mungu aliweza kusimamisha jua kwa ajili ya Yoshua kuwashinda maadui zake, kwa sababu aliamini. Mungu anaweza kusimamisha jua kwa ajili yako kuwashinda maadui zako, ukiamini. Mungu anapokuwa na wewe matatizo yako yako matatizoni.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Geuza matatizo yako kuwa changamoto, kuwa abra.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Abra maana yake ni fursa. Kwa hiyo, geuza matatizo yako kuwa fursa. Lakini, utageuzaje matatizo yako kuwa fursa? Kugeuza matatizo yako kuwa fursa, amini kama unaweza, usitumie muda mwingi kufikiria tatizo, tumia muda mwingi kufikiria fursa. Ukipata tatizo usikate tamaa. Badala yake, geuza tatizo hilo kuwa faida.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Vita ya Shetani na Mungu inatuathiri zaidi sisi wanadamu – na hapo baadaye itamuathiri Shetani pia. Vita hii haiwezi kuisha hadi siku ya mwisho, Yesu Kristo atakaporudi kuwachukua wateule wake. Pambana kwa njia ya maombi hadi siku ya mwisho kwa sababu adui tunayepambana naye hana muda wa kupumzika. Pambana kujiombea na kuwaombea wengine waliohai, na hata wale ambao bado hawajazaliwa, kabla mafuta ya dunia hii hayajalipuka. Usiishi kama adui wa msalaba wa Yesu Kristo, badala yake, ishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Kuishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo ni kupinga majivuno yote ya Shetani kwa upendo uliotukuka wa kujishusha au kujidharirisha, kutokutetereka hata kidogo na tamaa za ulimwengu huu kwa upendo mkubwa wa umaskini, na kutokuyumba wakati wa matatizo kwa sababu wakati wa amani ulijilimbikizia imani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kabla hujapona matatizo yanayokusumbua ponya roho yako kwanza, kabla hujakwenda kwa mchungaji, roho yako inajua kila kitu katika maisha yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tunapaswa kuyafikiria madhaifu yetu na dhambi zetu kwa makini sana, kwa kiasi cha kuyashinda madhaifu hayo na dhambi hizo, kabla hatujatoa maamuzi makali dhidi ya wenzetu. Tunawezaje kumlaumu mtu wakati hata sisi wenyewe tunaweza kuwa na matatizo makubwa? Tusiwe wanafiki. Badala ya kulaumu, saidia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa raha ni rahisi kuliko kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa shida, na utahitaji imani kuendelea kumwamini wakati wa dhiki. Vipindi vigumu katika maisha yetu hutokea kwa kila mmoja wetu. Kuamini ya kwamba Mungu ana makusudi ya lazima kukuondolea vikwazo katika maisha yako ni vigumu sana wakati mwingine, lakini imani ndicho kitu cha muhimu zaidi unachotakiwa kuwa nacho katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa. Amani ya Mungu, ambayo huzidi hekima na maarifa yote ya kibinadamu, ni kuliamini neno la Mungu kwamba ni la kweli. Bila imani hutaweza kumfurahisha Mungu. Imani ni ufunguo wa nguvu, uwezo na neema ambavyo Mungu ametupangia. Kwa ufupi, Mungu ni mkubwa kuliko wewe na matatizo yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Watoto wadogo wanakufa. Watu wazima wasiokuwa na hatia wanakufa vitani na katika majanga mengine ya asili. Kwa nini? Watoto wadogo wanaokufa walikuja duniani kufanya nini? Kwa nini watu wasiokuwa na hatia wanakufa ilhali Mungu yupo na asiwaepushe na matatizo ya dunia hii? Kama aliweza kuzuia binadamu wasiishi majini kwa sababu watakufa kwa nini asizuie matatizo yasiwapate watoto na watu wazima wasiokuwa na hatia? Sisi ni wadogo sana na Mungu ni mkubwa mno. Jibu hatutaweza kulielewa pamoja na kwamba tumepewa. Hata hivyo, Mungu hababaishwi na mwili. Anababaishwa na roho.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu ni mkubwa kuliko jumla ya matatizo yote na vitu vyote alivyoviumba na ana uwezo wa kufanya kila kitu alichosema atafanya bila kupunguza au kuongeza chochote. Usidanganywe na matatizo. Amka, kabla kifo hakijakufika.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Licha ya matatizo yanayotokea tunapaswa kujua kwa imani kwamba Mungu asiyeonekana na mwenye nguvu bado yuko kwenye kiti chake cha enzi, akisimamia kila kitu kinachoendelea, huku akijua bayana kwamba mapenzi yake lazima yatimie, bila kujali watu wasiomwamini wenye upofu wa rohoni.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Watu wote ni wa Mungu, watu ni matatizo. Wewe huna mtu, lakini bado unapambana na Mungu kuhusu watu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Matatizo tunayopitia si matatizo kwa ukuaji wetu. Mungu hafanyi hivyo eti kutukomoa. Anafanya hivyo kwa faida yetu ya baadaye.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kinachosababisha tupambane na Mungu ni matatizo, ambayo huletwa na watu, na tunapambana kwa silaha ya uongo.”
Enock Maregesi

« previous 1